St.Joseph Hospital Kagondo


HOSPITALI YA MTAKATIFU JOSEPH KAGONDO

KCMC Image

KCMC Image

KCMC Image

YAHUSUYO HOSPITALI YA MTAKATIFU JOSEPH KAGONDO. (IJUE HOSPITALI YA MTAKATIFU JOSEPH KAGONDO)

Hospitali ya Mtakatifu Joseph Kagondo ni taasisi isiyo ya kibiashara inayomilikiwa na Jimbo katoliki la Bukoba, katika Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Hospitali hii ilianzishwa na Wamisionari wa Afrika, ambao ni Mapadre na Masista (White fathers and White Sisters) mwaka 1912. Ilianza kama Zahanati na taratibu ilikua na kuwa hospitali kama inavyoonekana kwa sasa. Hospitali inapatikana upande wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, karibu na ziwa Victoria. Hospitali inafikifika kwa urahisi kutoka katika barabara kuu ya kutoka Bukoba kwenda Mwanza. Wagonjwa wanaotibiwa hapa wanatoka katika Mkoa wa Kagera, lakini mbili ya tatu wanatokea katika Wilaya ya Muleba. Wilaya ina eneo lakilometa za Mraba 11,000. Kati ya eneo hili, kilometa za mraba 7,925 ni maji. Wilaya ya Muleba ina Jumla ya watu 637,659 kadri ya sensa ya mwaka 2022.

Kulingana na sehemu inapokutwa hospitali ya kagondo, watu wengi wanapenda kuja kutibiwa kaitika hospitali hii maana inafikika kwa urahisi, ipo karibu na barabara kuu. Hospitali ya Mtakatifu Joseph Kagondo ina Wafanyakazi 150. Ina uwezo wa vitanda 160 vilivyosajiliwa na vipo katika wodi ya Wanawake, Wanaume, watoto na akina mama wajawazito. Hospitali inatoa huduma kupitia kliniki ya kisukari, Shinikizo la damu, huduma za afya ya uzazi na watoto, huduma ya wagonjwa wenye upungufu wa kinga za mwili na tiba yake na huduma za mkoba.

Pia kuna kitengo cha upasuaji, kitengo cha mazoezi ya viungo na utengenezaji wa viuongo bandia, kitengo cha kutengeneza dawa za vimiminika za kupitia kwenye mishipa ya damu, kitengo cha meno, maabara, famasi, na kitengo cha mionzi. Kwa njia za huduma za mkoba tunatembelea vijiji jirani ili kufundisha watu juu ya kutunza afya za watoto na faida za kuwapatia chanjo. Wajawazito wanapata ushauri juu ya utunzaji wa mimba na juu ya kujifungua kwa usalama wakiwa hospitalini.

Hospitali inatoa huduma za kibingwa za upasuaji wa mifupa kwa muda wote na kutengeneza viungo bandia. Pia hupata madaktari bingwa wa sikio, pua na koo kila baada ya miezi 3, na madaktari bingwa hawa hutoka katika hospitali ya rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.

Shughuli za kila siku za hospitali zinaratibiwa na Mganga Mfawidhi, Muuguzi Mkuu wa hospitali na Afisa tawala. Hospitali inaendeshwa kwa asilimia kubwa 80% na malipo ya wagonjwa wanaohudumiwa, kiasi kingine kinachangiwa na serikali kwa baadhi ya shughuli zilizoainishwa 15% na nyingine 5% inatokana na wafadhili wanapopatikana.

HUDUMA ZITOLEWAZO HOSPITALINI KWETU

KAGONDO NEWS
07/11/2025

HUDUMA YA KUUNGA MIFUPA

KAGONGO NEWS
17/10/2025

HUDUMA YA VIUNGO BANDIA

KAGONDO NEWS
07/11/2025

AFYA YA UZAZI NA MTOTO (RCH)

KAGONDO NEWS
07/11/2025

KLINIKI YA KINYWA NA MENO

KAGONDO NEWS
17/10/2025

UPASUAJI MKUBWA NA MDOGO


KAGONGO NEWS
17/10/2025

VIPIMO NA MATIBABU YA KAWAIDA

KAGONDO NEWS
07/11/2025

HUDUMA YA X-RAY

KAGONDO NEWS
17/10/2025

PHARMACY


KAGONDO HOSPITAL COLLABORATORS AND PARTNERS